Kutokana na mapenzi niliyokuwa nayo kwa mwanamzkiii huyo na alivyokuwa anapendwa na washabiki wengi haina budi kuuliza yuko wapii?
Ni yule yule DOCTOR MUUMINI ni yule kijana hodari kocha wa dunia.......hahaha hiyo ni sehemu tuu ya nyimbo ya mwanamuziki huyo,ambaye alitingisha tanzania nzima kwa sauti yake nzuri,lakini hivi sasa sijui yuko kwa wapi kwa maana mmh,ndo maana wahenga walisema ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka.huyu kijana alikuwa ni mtunzi mzuri na muimbaji mzuri wote tunalikubali.
Nikiwa kama mshabiki wa nyimbo zake na huwa nazisikiliza mpaka leo hii,huwa sichoki kusema kipaji anachooo ooh nimekumbuka alikuwa nacho sababu sijui sasa hivi kipo wapi au amekimbia wazaire hhahaha.Mpaka hivi sasa huwa sichoki kusikiliza TUNDA SPECIAL,MGUMBA,na nyinginezo.
Ombi langu linaenda kwa wamiliki wa bendi na maproducer jamani,muoneeni huruma mtaanzania mwenzenu kama aliwakosea,ni mtoto kukosa ni kawaida msameheni na mumrudishe studio,,,,,hahahaha...............Na wewe kaka MUUMINI acha ujuaji wakati sauti bila bendi ni sawa na kasuku anasauti nzuri lakini wimbo wake haunogiiiiiiiiiiiiiiiiiiii............peke yako huwezi kutokaaa au bora uanze kuimba bongo freva.....sipati picha maana nako kugumu mnooo
Jan 19, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment