Jijini dar au bongo kama inavyojulikana na wengi,kwa hivi sasa watu wanapewa buree chakula ni raha tupu kama si karaha.
Watu wa jijini mwa kandoro,wamebahatika kupata nafasi ya pekee ya kupata chakula bure bila kulipia hata shilingi mmoja.baadhi ya watu wanaweza wakasema wanabahati na wanapendelewa bora na wao waende jijini.lakini siku zote huwa vyabure vinamazara jamani,wala msipoteze nauli zenu kukimblia bureee hiyo.
Najua wengi wenu mtataka kujua ni chakula gani watu wa bongo wnapewa bure ,utakuwa unajiuliza ni MAHARAGE?UBWABWA?UGALI?AU MAKANDE?hahahha maana ndio kinapendwa na wengi.hapana wenzenu wanapata chakula ambacho kinamadhara baadae,je unajua ni kipi?Usione wala kudhani wanabahati ukalalamika kuwa JK mbona kwasahau na nyie.
kiukweli na kwa ufahamu wangu mdogo.wakazi hawa wanapata chakula cha vumbiiiiiiiiiiiii tuu kutokana na utengenezwaji wa barara usio isha.tunajua ukifika msimu wa maembe huwa kunakuwa na kipindupindu kwa wingi watu wanakuwa wanaurafiki na choo,lakini kwa kula vumbi watapata choo cha smenti kama si zege.poleeeni sana sasa ni wakati wa vijini kula raha.
Jan 20, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment