Jan 19, 2009

MITINDO MINGINE ACHA IKUPITEEEEEEEEEEEEEEEEEE SHOSTITO


Mtu akikupenda na akikujali ndio atakae kuambia ukweli hata ukikuuma au laah,lakini akikuacha bora liende ujue hana mapenzi na wewe.
Kilichopelekea kuandika habari hii ni baadhi ya tabia ya watu kutoangalia kipi kinawafaa kutokana na miili yao,wao huvaa tuu bora kitu kipo kwenye chati hata kama ni kituko kwao.
Hivi sasa kila msichana utakaemuona mjini anataka kuonyesha kiuno chake,hata kama kiuno kipo juu kama kamba au hana kiuno au ana wowowo kuubwa sana.kiufupi huu mtindo wa kuvalia nguo chini ya kiuno haujawekwa kwa wote jamani,kizungu wanaita low cut,ni kwa ajili ya wale wasio na nyama za mgongo,waliokatika kiunoni na wasio na wowowo kabisa.hii inakera sana unapotembea mjini unamuona mwanamke mwenzio kaachia vitu nje huku baadhi ya vijana wakimcheka na mwisho wa siku unajiona hata wewe usievaa hivyo unapata aibu kwa niaba yake.
Kwa kumuangalia tu mtu wa aina hiyo,huwa unajiuliza hivi huko nyumbani kwake anakaa peke yake?au ana msichana wakazi ambaye anamuogopa boss wake kumueleza ukweli na kubaki anamchekea tumboni?au kioo chake kinamuonyesha sura tuu?
Ndipo hapo niaposema mitindo mingine iache ikupite jamani kwa maana kila mtindo una mtu wake haujaumbwa kwa wote,kuliko kuadhirika ni aiibu tupuuuuuuuuuu.yenu hiyo warembo......................................

No comments:

Post a Comment