Jan 22, 2009

MAISHA MAFUPI YENYE STAREHE YAMEMALIZA WENGI MJINI

Wenye mji wenyewe wanausemi wao siku hizi,bora waishi maisha mafupi yenye starehe kuliko marefu yenye shida...........................
Kwa mwendo huu atapona mtu kweli?mpaka kufikia hapo ujue watu wameamua tayari kujilipua kama si kujitoa muhanga ,yani lolote na liwe bora mambo yangu yawe safi.sijui hawajiulizi yawe safi kwa muda gani maana wanafikiri miaka kumi mbele pasipo fahamu inaweza ikawa mwaka na nusu......haaaaaaaaaaaaaaaaa.
Imekuwa ni kama tabia jijini kwa wasichana na wavulana,kufata mtu kwa ajili ya mfukoni mwake kukoje,haijalishi uyo mtu afya yake ikoje? wao bora chapaa au pesa tuu,ukimuuliza unamjua? ooh utajibiwa nimjue kwani ndugu yangu na kwamba wao wanaangalia pesa na usafiri.Jiulize sasa yale matangazo yote ya ukimwi watu hawayaoni?au wanaona ni matangazo ya pipi kifua?
Inasikitisha sana kuona watu wanadanganyika kwa usafiri na pesa,na kupelekea kutojali afya zao,sasa huu ugonjwa wa ukimwi kwa mwendo huu,utaisha kweli?Ukiwaona mjini wanatembelea magari mazuri, wenyewe wanasema wanatesa,jiulize kutesa uko kwa muda mfupi kwa nini?maana mwaka bararani miaka miwili kitandani.......Ndio wameamua sasa maisha mafupi yenye starehe...........Ila mnaowatesa ni wachache na mtawaacha kwa tamaa zenu za maisha ya juu.

No comments:

Post a Comment