Swali hili wamekuwa wakiulizana watu mbali mbali, na wengine kutuambiana kuwa, wao wanaokaa masaki ni watoto wa geti kali na wahali ya juu kwa ujumla mambo safi,wakati wanaokaa mbagala wanaitwa kuku wa kienyeji yaani wasiofugika au watoto wa uswahilini.
Kama kawaida ya kwa nafasi huwa tunaweka vitu bayana,haswa vile vya ukweli.kwa upande wangu kwa kuwaangalia tuu hivi kwa machoni siwezi kujua yupi anatokea mbagala na yupi anatokea Masaki,pasipo kuambiwa na mtu kuwa huyu ni wamasaki na huyu ni mbagala...nikasema nisikilize wenyewe wakazi wa maeneo hayo.Nilibahatika kuanza kukutana na watu wa masaki na haya yalikuwa ndio majibu yao,Nani asiejua kuwa watu wa masaki ndio wanaongoza kwa kuwa na hela,,,,mmh hapo nikajijibu kwenye nafsi yangu watu wa mbagala kwahiyo hawana hela?....mmh nikasema sasa wanatumia nini?pili watu wamasaki wengi tunaendesha magari,,.....mmmmh haya lakini moyoni tuu najijibu,tatu Nyumba zetu ni nzuri na safi,......hapo kidogo kuna ukweli lakini kwenye usafi....nne kuna maghorofa mengi.....hee nikasema sio ya serikali lakini....tano Hakuna wakabaji huku wala wabakaji.......mmh nikasema watoke wapi wakati kuna nyumba za wakubwa wa nchi nyingi,,,,,,.....Sita umeme huwa haukatiki ovyo......hii kweli,,,,sababu hakuuzwi bangi huku zaidi ya bia na sigara...............sasa kwahiyo mbagala hakuuzwi bia,wanauza nini gongo?,,,mweeeeh....nikasema hayo nimeyaskia sasa wambagala wao wanasemaje?
Skia ndugu mwandishi,kwanza nikufahamishe uku mbagala nyumba ni zakwetu wenyewe hakuna ya buree huku,wala ya kulipa mwisho wamwezi laki mmoja mpaka umalize deni ndio nyumba iwe yako........nikasema heee mboni wanapiga kwenyewe.....kuhusu usafi je unasemaje,,,,,,bwana weee nyumba ni zakwetu wenyewe sasa usafi huo wanaoutaka wao ni upi wakupaka rangi nyumba au?nikasema watu wa huku wanaongea sana mmmh.....je kuhusu kuwa na magari?mmh hawaoni huku pia kunafoleni kwenda mjini nakurudi kama hakuna magari foleni ya nini?nikasema kazi kweli kweli....vipi kuhusu umeme kukatika ovyo uku kwenu,,,,sie hilo si tatizo kwetu sababu tunatumia sana umeme wa asili....hapo kidogo nikaogopa,,..je wakabaji na wabakajii,....weeeeeeeeeee uku hamna vya hivyo kila unaemuona anasilaha yake nani atamsogelea alafu uku tunajuana.....mmmhkazi kweli kweli....
Kwa kuwasikiliza watu hawa,nimeona jibu ni mmoja tu kila mtu anapenda kwake na kusifia kwake,na kwa majibu yao,yameniweka njia panda mpaka mimi sijui wewe msomajii wa habari hii,mi naona ni drooooooooooooooooooo au wenzangu mnaonaje? comment kwa chini hapo
Jan 22, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment