
Tangazo jamani,kwa wote wenye mawasiliano na kijana huyu na wanaepajua wapi anapatikana,ili tuwasaidie watoto wetu ambao ni taifa la kesho.
Kijana huyu anajulikana sana kwa kuwaburudisha watoto na watoto pia huwa wanampenda sana mpaka kumtafuta na kuwa na hamu ya kumsikia kijana huyu.Sio mwingine ni MR NICE au mzee wa kidali poo kama anavyojulikana na wengi.
Mwanamziki huyu ambae alikuja na staili yake ya takeu na kuimba nyimbo nyingi za watoto na ambazo zilikuwa zinachezeka sana na yeye mwenyewe akiwa mchezaji mkubwa sijui amefia wapi kama sio kufichwa.Nimekaa nikajiuliza kuwa vipi mbona haimbi tena,jibu la kwanza likawa au anamuogopa ZE DUDU BAYA?AU KIKOSI CHA MIZINGA?Nikasema hapana kwa kuwa wapo watu wakumlinda yaani,polisi kama si wanajeshi.Jibu la pili likawa ooooooooooh NYIMBO ZOTE ZA WATOTO KAZIMALIZA haaahhahahahhaah,nikasema kuna ukweli hapo.
Natumia nafasi hii kumbusha kuwa upo wimbo wa watoto mmoja kausahau nao ni KICHURA CHURA mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh,......Haya nenda studio NICE wimbo huo....teheeeeeeeeeeee
No comments:
Post a Comment