
Mhhh hii haijakaa vizuri kabisa na inakera watanzania wengi na wasikilizaji wa r
adio maarufu jijini bongo na mikoani.
kutokana na wapenzi wengi na wasikilizaji wa radio clouds kupenda sana kusikiliza kipindi cha POWER BREAKFAST,kilichokuwa kinaendeshwa kwa ustadi zaidi na kufanya watu wengi kukipenda hapo zamani wakati kilipokuwa kinaendeshwa na FINA MANGO NA MA
SOUD KIPANYA hivi sasa hali imekuwa kunyume kabisaaa.
Na ndo maana nikasema ufundi ukizidi huwa unaharibu,kwa matazamo wangu tuu bila kuhitaji mtu wa kujua kilikuwa kinaingiza kiasi gani? na asilimia ngapi ya watu waliokuwa wakikipenda kwa ujumla, kwa upande wote ni zaidi ya asilimia mia moja.lakini hivi sasa kipindi kimekuwa kibaya,hakifurahishi,hakina jipya ni bora kipindi.wakati huo lazima mtu ulikuwa uamke saa kumi na mbili kamili uanze kuwasikiliza na kujua kinachoendelea katika dunia.lakini hivi sasa huwa wala mtu hushtuki ukilala ukiamka ni jahazi limeanza au leo tena.sasa najiuliza hivi huwa mtu ukisifiwa sana au ukipendwa sana au ukijiona wewe ndo zaidi lazima uharibu?
Kwa hivi sasa huwa sioni wala sifikirii kipi cha kusikiliza siku za kawaida katika radio hiyo ambayo kwa sasa inaongoza kwa kusimamisha watangazaji,zaidi ya kusubiria jumapili kumsikiliza GEA HABIBU na kipindi chake cha taarabu au kusubiri michezo basi siku ipite.
Nimekaa na kutafakari hivi huwa mwaka ukiwa unaanza au mwaka ukiwa unaisha unaisha na kila kitu au ndo lazima kuwa na mabadiliko?Basi kwa mabadiliko hayo na ubunifu huo ni sawa na kupika ugali na kuufunika ukaula baada ya masaa mawili,si utakuwa umeota koti?
Wazee wa zamani wanasema siku zote huo unajifunza na yaliyopita lakini kwa radio hiyo naona NI UFUNDI MWINGI SASA WANAHARIBU.TEHETEHEEEEEEEEEEEEEE
No comments:
Post a Comment