Jan 14, 2009

mmh bongo sasa ni yebo yebo tuu


bongo ni yebo yebo kwa kwenda mbele.
Nawapa taarifa wale wageni wanaoenda jijini dar,wakiwa wanatokea mikoani na uko ulaya,kumbukeni kubeba nguo za njao jamani ili muonekane hampo nyuma katika mavazi.wote tunajua kitu kikiingia bongo kinavyokera sasa hivi basi ni rangi ya njano,kila kona utakayokatiza ni njano tuu ukiwa muoga utaogopa nakudhani kuna kitu kinaendelea au yanga inacheza au manji kashusha vitu vya bure hahaaa,hpana ni mapigo tuu.

Sasa nduguzanguni tuelezane vizuri na kabla aujatokaa nyumbani jiangalie kwanza hiyo njano yako jamani,kuna nyingine bora ni njano ila ni mbaya na mnaumiza wenzenu macho au mnataka wakina matonya waongezeke?maana unamkuta mtu kavaa njano tele kwenye mwili kumuangalia mpaka unaona aibu eeh na kuogopa jinsi macho yako yatakavyozulika.
tunaelewa kuwa kitu kikiwa moto na watu wanakuwa moto ila huu moto wa kuvaa njano mwili mzima mmh aujatulia kabisaaa.

Ingawa ndiyo color of the year lakini msijewafanya watazamaji wakajutia kwanini rangi hii imechaguliwa kuwa rangi ya mwaka, vaa njano lakini tena isiwe manjano....maana wengine utakuta top njano, viatu njano, hereni na mabangili njano, mkanda njano, Handbag njano, vibanio vya nywele njano....inachefua. Mtatuumiza wenzenu kumtwari...

1 comment:

  1. hiyo nimeukubali kabisaa.nimepita juzi kariakoo bado kidogo nigongwe na gari kwa kuwa nilikuwa sioni baana ya kuingia duka moja limejaa nguo za njano tuu tena mbayaaa

    ReplyDelete